Tuesday, 17 November 2015

wanawake wapewa talaka zanzibar kwasababu ya kukiunga chama cha mapinduzi

Image copyrightZanzibar Electoral Commission
Image captionKuhesabiwa kwa kura Zanzibar wakati wa uchaguzi mkuu uliopita
Takriban wanawake 14 kutoka kisiwani Zanzibar nchini Tanzania wanaotuhumiwa kukiunga mkono chama tawala cha mapinduzi CCM katika uchaguzi uliopita kinyume na matakwa ya waume zao wamepewa talaka.
Kulingana na gazeti la Zanzibar daily Newspaper.
Watalakiwa hao wamesema kuwa wanaume zao waliamua kuwapatia talaka nyakati tofauti kutokana na tofauti za kisiasa kwa mujibu wa gazeti hilo.
Limeongezea kwamba wanaharakati kutoka kwa muungano wa mawakili wanawake kisiwani pamoja na mungano wa wanahabari wa kike nchini Tanzania wamesikia kuhusu visa kama hivyo na wameahidi kufuatilia swala hilo.

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...