Thursday, 15 September 2016

mapenzi matamu ila yanadanganya, soma stori hiyo..

Nina msichana ambaye nimempenda sana, ni muda kitambo nimekuwa nikiwasiliana naye kama rafiki yangu! Kiukweli huwa tunachat naye sana, hana kinyongo kabisa! Kuna siku nilimkosea baada ya kumtania nina mtu mwingine, kesho yake hakuwa na hamu kabisa ya kuchati na mimi, kila nilipomwambia kitu alitengua na kudai anaumwa au amechoka au anajisikia vibaya! Ukweli ulikuja kubainika kuwa nilikuwa namtania tu na haikuwa kweli. Alifurahi sana tuliendelea kuchati kama kawaida yetu!

Muda umeenda mwishowe nikaamua kumweleza kuwa nampenda ili awe mke wangu! tulipanga siku ya kukutana na kuzungumza nae kuhusu hilo. Usiku wa kuamkia siku yenyewe aliniuliza kama nina mpenzi au nilishawahi kuwa na mpenzi, nilimwambia nilishawahi akaniuliza kwann mliachana nikamwambia alikuwa mwanafunzi so sipenbdi kumharibia masomo as why nilimuacha! Nilipomuuliza yeye kwanza alikataa kuniambia, lakini katika kumuomba aniambie aliniambia anamchumba ambaye anampenda sana na amejikommiti kiukweli kwake ila aliniambia hivi: ananipenda sana ila hana jinsi! mchumba wake hawajajitambulisha home kwao wala kulipa mahari, just uchumba wa vijana wa siku hizi! Aliponiambia hivyo niliumia sana nikaamua kupotezea, kesho yake mapema sana aliniandikia message nzuri sana iliyonifurahisha! nikaendelea kuchati nae. siku ya siku ilipowadia sikusita nilimweleza upendo wangu na kumwambia ukweli kuwa namhitaji sana awe mke wangu! Aliniandikia message baadae akasema amefurahi sana!

Nimejaribu kila wakati kutaka kujua hatima sasa, mara nyingi anasema hana jinsi au anashindwa afanyaje au sio rahisi maneno ya kuonyesha tu kuwa anampenda sana jamaa! Amekuwa akionyesha love yake kwa action tu lakini kwa mdomo kusema YEs hata siku moja!

1. Sasa je, huyu demu ananipenda kweli au ni mchezo tu mapenzi?
2. Nifanyeje sasa ili nikubalike na kupewa utawala na hatimaye kumuoa?

Natanguliza shukrani

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...