Baada ya michezo nane kuchezwa
usiku wa Septemba 13 2016, Jumanne ya septemba 14 michezo 9 ya hatua ya
makundi ya michuano ya klabu Bingwa barani Ulaya ilichezwa barani Ulaya,
miongoni mwa michezo iliyochezwa usiku wa Septemba 14 ni pamoja na
mchezo wa Real Madrid dhidi ya Sporting CP.
Sporting CP ni klabu ilimyolea Cristiano Ronaldo kutokea academy yao, hata hivyo hiyo haikuwa mechi rahisi kwa Real Madrid
kwani walifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-1 ila walilazimika
kusubiri hadi dakika ya 90 kujihakikishia ushindi huo kupitia goli la
kichwa la Alvaro Morata ikiwa ni dakika moja imepita toka Ronaldo asawazishe goli.
No comments:
Post a Comment