MADHARA KWA MWANAUME.
1.Kupata maambukizi katika njia ya mkojo hadi kwenye kibofu.
2.Maambukizi katika
tezi dume(Prostetits) hii inaweza kuathiri mfumo wa uzazi wa mwanaume.
3.Kuziba kwa njia ya
mkojo.
4.Utasa au ugumba.
5.Ulegevu wa misuli
ya uume na upungufu wa nguvu za kiume.
6.Athari mbaya ya
kisaikolojia kwa kuwa anafanya tendo katika mazingira machafu hali
itakayompelekea kutolifurahia tendo kutokana na hali ya umaji maji,utelezi, au
harufu kali na mbaya na hivyo kuona kuwa mwanamke ni mchafu.Pia hali hii
ikizidi inaweza kuathiri hata hufanyaji wa tendo katika siku za kawaida sio za
hedhi.
MADHARA KWA MWANAMKE.
1.Kupatwa na mambukizi viungo vya ndani vya uzazi kama vile
shingo ya kizazi,mirija ya uzazi kwa ujumla wake anaweza kuwa na tatizo la PID(
PELVIC INFLAMATORY DISEASES) tatizo ambalo linaweza kuathiri mfumo wake wa uzazi.
2.Maumivu makali ya
tumbo hasa kwa wale wanaopatwa na maumivu wakati wa hedhi.(Dysmenorrhea).
3.Utokaji wa damu
unaweza ukaongeza kuliko vile inavyotoka kwa kawaida yake.
4.Utasa au Ugumba.
5.Kuvimba kwa kuta za
ndani za uke kwa kuwa wakati wa hedhi zenyewe huwa tayari zimevimba au
kutanunuka hali pia itamsababishia maumivu kwenye uke wakati wa tendo la ndoa.
6.Athari mbaya ya
kisaikolojia:Mwanamke atahisi kuwa mumewe hamjali wala mpendi bali anajali
hisia zake za kingono na kwamba yeye anatumika kingono tu.Pia kuona kuwa mumewe
ajali afya yake pamoja na maumivu anayoyapata lakini bado huyu mume anataka
KU-DO.
NOTE
Hali hii ikizidi
inaweza kuathiri hata hufanyaji wa tendo katika siku za kawaida sio za hedhi.
No comments:
Post a Comment