Monday, 22 May 2017

BAADA YA KUTOLEWA AFCON, KWA MUJIBU WA TFF HIKI NDICHO WATAKACHOFANYA SERENGETI..




Safari ya Serengeti Boys - timu ya Tanzania ya Vijana wenye umri wa miaka 17, inaendelea licha ya jana Mei 21, mwaka huu kuondolewa kwenye hatua ya makundi ya kuwania taji la Afrika hapa Port Gentil nchini Gabon.


Serengeti Boys ilifungwa bao 1-0 na Niger katika mchezo uliofanyika , hivyo kufanya matokeo ya timu zote mbili kufanana kwa pointi, idadi ya mabao ya kufunga na kufungwa tangu kuanza kwa fainali hizi za AFCON, Mei 15, mwaka huu.


Serengeti Boys ilikuwa Kundi B pamoja na Mali iliyoongoza kundi hilo kwa kufikisha pointi saba, ikifuatiwa na Niger yenye pointi nne sawa na Tanzania pamoja na Angola iliyoambulia pointi moja.


Licha ya Serengeti Boys kulingana na Niger, lakini wapinzani wa Tanzania walipenya kwenda hatua ya nusu fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika kwa faida ya ushindi katika mchezo ambao umekutanisha timu hizo.


Kanuni hiyo ya mashindano ya CAF inajieleza kuwa matokeo ya ‘head to head’ kwa maana zinapokutana timu mbili zenye uwiano wa pointi na magoli kinachoangaliwa hapo ni timu gani ilimfunga mwenzake walipokutana na ndipo matokeao hujulikana,

Kwa jana Mei 21, mwaka huu hali hiyo ilijitokeza hivyo Niger kusonga mbele kwa kuwa aliifunga Tanzania bao 1-0 katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Prt Gentil nchini Gabon.

Akizungumzia matokeo hayo, Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amesema: “Kuvunjika kwa koleo si mwisho wa uhunzi.”

Alizungumza hayo kwa nyakati tofauti, Malinzi alisema: “Tujipange sasa kwa yafuatayo: Michezo ya kufuzu (Qualifiers za 2019 Afcon U20  zinafanyika mwakani kuanzia mwezi June. Vijana hawa watashiriki.

“AFCON U17 finals (Fainali za AFCON za vijana wenye umri wa chini ya miaka 17) zinafanyika Tanzania mwaka 2019,” amesema Malinzi na kuongeza: “Serengeti Boys hii ya sasa inakuwa Ngorongoro Heroes (Vijana wa u20 na ikishapumzika kwa muda, itaingia tena kambini.”

Amesema kwamba vijana wa Tazania wenye umri wa chini ya miaka 15, walioko Shule za Alliance Mwanza wanakuwa Serengeti Boys wapya.

“Hakuna muda wa kusononeka ni kuchapa kazi tu. Kikubwa tunaandaa Taifa stars ya kwenda World cup 2026 na qualifiers zake zitaanza mwaka 2024. Kwa sasa timu inajiandaa kuingia kambini kwa ajili ya kuivaa Lesotho,” amesema.


Kocha Mkuu wa Serengeti Boys, Bakari Shime amesema timu yake imepoteza mchezo huo kwa makosa ya kimchezo na bahati haikuangiwa kwa vijana wa Tanzania katika mchezo dhidi ya Niger.
source: salehe

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...