Monday, 22 May 2017

Chelsea na Sunderland matatani kwa kupanga mechi

Chelsea wamebeba ubingwa wa mara ya 5 katika ligi kuu, hakika wiki hii ni nzuri kwao na pia kwa kocha wao Antonio Conte kwa kuwa wana jambo kubwa la kujivunia.
Lakini sasa Chelsea wameingia matatani baada yakubainika kwamba mchezo wao wa mwisho dhidi ya Sunderland waliupanga kabla ya mchezo kuanza.
Sheria za chama cha soka Uingereza zinasema “hairuhusiwi kupanga matokeo, au mashindano au tukio lolote katika mchezo huo kinyume na mipango ya chama cha soka”
Sasa wakati wa mchezo kati ya Chelsea na Sunderland, mlinzi mkongwe wa Chelsea John Terry alitolewa uwanjani baada ya kucheza uwanjani kwa dakika 26 tu, swali likaja sub hiyo inatokeaje dakika ambayo ndio namba ya jezi ya Terry?
Baada ya filimbi ya mwisho kocha wa Sunderland David Moyes alikiri kwamba kulikuwa na mpango maalum kumuaga Terry ambapo dakika ya 26 wangeufanya mpira usimame ili afanyiwe sub.
Chelsea inaonekana walifanya makubaliano na Sunderland kabla ya mchezo huo ili kutekeleza jambo hilo dakika ya 26 namba ambayo ndio namba ya John Terry.
Inaonekana golikipa wa Sunderland Jordan Pickford na Diego Costa walijua nini wanatakiwa kufanya mpira ukifika dakika ya 26 na kuutoa mpira nje ili Terry apewe heshima katika dakika hiyo ya namba yake ya jezi.
Hadi sasa haijafahamika wazi ni hatua gani FA wanaweza kuchukua kuhusiana na tukio hilo lakini kuna tetesi zinadai kwamba FA wameamua kuachana na tukio hilo na wanaweza wasilichunguze.

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...