Monday, 26 June 2017

john bocco kuchukua jezi namba ya Muzamiru?

Muzamiru YassinMuzamiru Yassin hana hiyana, amesema atakuwa radhi kumpa John Bocco jezi yake nambari 19 ikiwa mchezaji huyo mpya ataitaka
Kiungo mshambuliaji wa Simba Mzamiru Yasini, amesema yupo tayari kumwachia namba 19 mshambuliaji mpya aliyesajiliwa na timu hiyo kutoka Azam FC, John Bocco na yeye kutafuta namba nyingine.
Mzamiru ameiambia Goal,  yeye mpambanaji hivyo namba yoyote anaweza kuvaa na akafanya vizuri hivyo haoni shida kumpa Bocco, jezi hiyo ambayo yeye aliweza kuitendea haki kwa kufanya vizuri na kuisaidia timu hiyo kuwaa ubingwa wa kombe la FA.
“Nipo tayari kumwachia Bocco namba 19, endapo ataihitaji, kwasababu ni rafiki yangu wa karibu sana lakini siku zote mimi huwa sichagua namba kwasababu ninayecheza ni mimi na siyo yenyewe,” amesema kiungo huyo aliyeifungia Simba mabao saba msimu uliopita.
Mzamiru amesema alipokuwa Mtibwa alikuwa akivaa jezi namba 10, na aliweza kufanya vizuri hata Simba kumsajili na hata alipotuwa Simba na kukabidhiwa namba 19, nayo ameweza kuitendea haki kwa kuipa mafanikio makubwa timu hiyo.
Kiungo huyo alisema anamkaribisha kwa upendo mshambuliaji huyo na anaamini atakuwa na mchango mkubwa kwenye kikosi chao msimu ujao hivyo na yeye atahakikisha anampa ushirikiano wa kutosha ikiwemo kumuachia jezi hiyo endapo ataihitaji.
Bocco amekuwa muumini mkubwa wa namba 19, ambayo mwenyewe anaamini ndiyo imekuwa na bahati kwake kwa kufunga mabao ya kutosha kila anapoingia dimbani.
Bocco amekuwa muumini mkubwa wa jezi namba 19, ambayo pia alikuwa akiitumia akiwa Azam hivyo Mzamiru amesema kama atamuafata na kumwomba hatokuwa na hiyana zaidi ya kumwachia mshambuliaji huyo ambaye anatarajiwa kufanya makubwa akiwa na kikosi cha Simba msimu ujao

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...