Monday, 26 June 2017

viungo wakabaji waliong'ara msimu uliopita

Viungo wakabaji waliong’ara msimu uliopitaGoal inakuchambulia baadhi ya viungo bora wakabaji kwa msimu uliomalizika wa 2016/2017
Ni nyota wachache wanaoweza kuimudu nafasi ya kiungo mkabaji kwa sasa kwenye Ligi Kuu Bara, tangu zipite zama za kina  Selemani Matola, Athumani Idd na wengine ambao walifanikiwa kuimudu nafasi hiyo ya kiungo mkabaji, sasa eneo hilo limekuwa likitesa klabu nyingi kwenye Ligi kwa kukosa watu sahihi
Kwa msimu uliomalizika wapo baadhi ya wachezaji walifanikiwa kucheza vizuri nafasi ya kiungo mkabaji, kwa asilimia kubwa walitimiza majukumu yao ya kuilinda safu yao ya ulinzi isipate madhara pindi wanapo shambuliwa na kuisukuma timu mbele wakati wakiwa na mpira
Goal inakuchambulia baadhi ya viungo bora wakabaji  kwa msimu uliomalizika wa 2016/2017

Ndiye kiungo mkabaji bora kwa sasa hapa nchini, anaongoza kwa kupokonya mipira , Himid nyota wa Azam na timu ya taifa Tanzania, amekuwa mzuri kwenye  kuilinda safu yake ya ulinzi isipatwe na madhara kwa kuzuia hatari zote, kiungo huyo amekuwa na nidhamu kubwa kwenye eneo hilo kuliko kiungo yeyote kwa sasa

Kiungo huyo amekuwa mzuri kwenye kupiga pasi fupi fupi na ndefu kwa usahihi bila kupoteza, Mkude amekuwa muhimili mkubwa ndani ya Simba katika eneo la katikati hasa la ulinzi na kuifanya timu iwe kwenye usalama pindi ikiwa inashambuliwa mara kwa mara

Licha ya umri wake kuwa mkubwa ila bado nyota huyo alifanikiwa kuhimudu nafasi ya kiungo mkabaji kwa asilimia kubwa tofauti na matarajio ya wengi, Nditi amekuwa imara kwenye utimamu wa mwili hasa ikitokea kwenye mipira ya kugombania dhidi ya timu pinzani

Kenny Ally (Singida United)
Amejiunga na Singida akitokea Mbeya City aliyoichezea msimu uliopita, Kenny ana sifika kwa uwezo wake mkubwa wa kupiga mashuti ya mbali, ni mzuri kwenye kusoma mchezo kwa haraka na kugundua udhaifu na ubora wa mpinzani

Nyota wa klabu ya Kagera amefanikiwa kucheza kwa ubora mkubwa kwenye eneo la kiungo mkabaji kila anapopewa nafasi kwenye eneo hilo, ana uweo wa kupiga pasi fupi na ndefu pia ni mzuri kwenye kukaba bila kufanya faulo hali kadhalika ana uwezo mkubwa wa kufunga, amemaliza na magoli zaidi ya matatu licha ya kucheza chini sana

Stephan Kingue (Azam)
Ukitaja wakata umeme kwenye Ligi msimu uliopita jina la Kingue haliwezi kosekana, alionesha umaridadi wake hasa kwenye mashindano ya Mapinduzi kabla ya kuumia, Kingue siyo mzuri sana kwenye kupiga pasi kama wengine ila ni shapu kwenye kufika kwenye tukio kwa haraka na kulizuia, pia ni mzuri kwenye kuzuia mipira ya juu kutokana na kimo chake

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...