Floyd Mayweather ametimiza pambano la 50 katika ngumi za kulipwa akicheza bila ya kupoteza.
Mayweather amempiga bingwa wa michezo ya UFC (ngumi na mateke), Conor McGregor kwa TKO katika raundi ya 10.
Mwamuzi alilazimika kuingilia na kusimamisha pambano katika raundi ya 10 baada yya kuona Mayweather anamuangushia kipigo kikali McGregor raia wa Ireland ambaye hakuwa akijibu kitu tena.
Hata hivyo, McGregor amewashangaza wapenda ngumi duniani baada ya kuongoza kuanzia raundi ya kwanza hadi ya tatu.
Kuanzia raundi ya nne, Mayweather alianza kucharuka na taratibu ilipofika raundi ya 7, ilionekana McGregor amepoteza mwelekeo.
Katika raundi ya 8, McGregor alionekana kuchoka hasa miguu, hivyo kutoa nafasi kwa Mayweather kumpiga ngumi nyingi zaidi zilizomfanya achoke zaidi. Huenda angeweza kujitoa katika raundi ya 9 lakini akaamua kuendelea raundi ya 10 ambayo ilimshinda kabisa.
wataalamu wa mambo wakaona ni dhahiri shahiri kwamba McGregor hatoweza tena kuendelea na pambano hivyo kumtoa katika machezo na kumpa ushindi Maywether.
No comments:
Post a Comment