Saturday, 12 August 2017

ousmane dembele apewa hadhabu na klabu yake

TIMU ya Borussia Dortmund imekataa ofa ya Barcelona kutaka kumnunua Ousmane Dembele kabla ya kumsimamisha kinda huyo kufuatia kutoonekana mazoezini Alhamisi ya jana.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20, ambaye amekuwa akitaja kama mchezaji anayefaaa kumrithi Neymar, amepigwa faini na amefungiwa kufanya mazoezi na wachezaji wenzake hadi wiki ijayo.
Baada ya kocha wa Dortmund, Peter Bosz kuthibitisha kwamba Dembele hakuhudhuria mazoezi Alhamisi, klabu ikatoa taarifa ikifafanua kwamba mshambuliaji huyo ametolewa ofa na Barcelona - moja ambayo ilikataliwa kwa sababu haiendani na uwezo wa hali ya juu wa mchezaji huyo.

Ousmane Dembele amefungiwa kufanya mazoezi na wachezaji wenzake wa Borussia Dortmund baada ya kutoonekana Alhamisi kufuatia kutolewa ofa na Barcelona PICHA ZAIDI GONGA HAPA 


"Borussia Dortmund ilifanya mazungumzo na FC Barcelona juu ya uhamisho wa mchezaji wa BVB, Ousmane Dembele kwenda FC Barcelona," imesema taarifa hiyo.
"Katika mkutano huo, wawakilishi wa FC Barcelona walileta ofa ambayo hailingani na kiwango kikubwa cha soka ya mchezaji wala hakilingani na thamani halisi ya sasa katika soko la wachezaji Ulaya. Pamoja na hayo, BVB ikaikataa ofa hiyo.
"Na kwa kuwa hakuna iliyoletwa na Barcelona hadi leo, kwa sasa hakuna mchezaji atakayehamishwa kwenda FC Barcelona,".
Baadaye Dortmund ikatoa taarifa ya pili ikielezea kitendo cha mchezaji kutohudhuria mazoezi ya Alhamisi bila taarifa na kumpiga faini sambamba na kumsimamisha hadi baada ya mechi ya Rielasingen Jumamosi.
Barcelona inamtaka Dembele kama chaguo la kwanza baada ya kumuuza mshambuliaji wake, Neymar kwenda Paris Saint-Germain kwa dau la rekodi ya dunia, Pauni Milioni198. 
Mkurugenzi wa Usajili wa Dortmund, Michael Zorc mapema wiki hii alikanusha taarifa kwamba dismissed Dembele amekubaliana na vipengele binafasi na  Barcelona.
Dembele aling'ara msimu uliopita katika Ligi Kuu ya Ujerumani, akifunga mabao sita na kujipatia nafasi katika kikosi cha kwanza cha Timu Bora ya Msimu wa Bundesliga.
Barcelona pia imetoa ofa ya Pauni Milioni 90 kwa kiungo wa Liverpool, Philippe Coutinho ambayo ilikataliwa Alhamisi

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...