Ligi Kuu England msimu wa 2016/2017 imejaa vivutio vingi au kuna majina mengi unaweza kusema yamefanya iwe na mvuto wa kipekee, ukiachana na upinzania wa Pep Gurdiola na Jose Mourinho, Zlatan Ibrahimovic wa Man United amekuwa kivutio pia kwa kauli zake anazopenda kuzitoa.
Ikiwa siku tatu zimesalia kabla ya ulimwengu wa soka kushuhudia Man City ya Pep Guardiola na Man United ya Jose Mourinho zikikutana, Zlatan amemtumia ujumbe na zawadi golikipa mpya wa Man City Claudio Bravo kabla ya mchezo wa jumamosi, Zlatanameonekana kupitia video fupi akifunga zawadi ya kufanyia mazoezi ya Bravo.
Video hiyo ya Zlatan ilyoambatana na maelezo ya “Karibu katika jiji la Manchester hivi ni baadhi ya vifaa vya mazoezi utahitajia, tutaonana jumamosi” huo ni ujumbe wa utani waZlatan kwa Bravo unaotafsirika kuwa kipa huyo aliyejiunga na Man City akitokea FC Barcelona ajiandae kwa mchezo wa jumamosi.
No comments:
Post a Comment