Thursday, 14 September 2017

Carlos Tevez aonywa na unene wake na kocha wake

Carlos Tevez
Mshambuliaji wa Argentina Carlos Tevez ameambiwa na mkufunzi mpya wa klabu yake ya Shanghai Shenhua nchini China Wu Jingui kwamba ni mnene na hatachezea timu hiyo hadi apunguze uzani na kuwa sawa kucheza.
Tevez, 33, ambaye anaaminika kuwa miongoni mwa wachezaji wanaolipwa pesa nyingi zaidi duniani, amefunga mabao mawili pekee katika mechi 12 tangu alipoanza kuwachezea mwezi Machi.
Wu, aliyechukua usukani katika klabu hiyo baada ya Gus Poyet kujiuzulu Jumatatu, pia alimkosoa kiungo wa kati qFredy Guarin.
"Ninafaa kuwajibika kwa timu na kwa wachezaji," alisema Wu.
"Wote wawili (Tevez na Guarin) wana uzani uliozidi kiwango. unapokuwa uwanjani, ikiwa huwezi kucheza 100%, basi haina maana."
Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United na Manchester City alihamia Shanghai kutoka Boca Juniors.
Hata hivyo alikosa karibu nusu ya mechi za klabu hiyo msimu huu kutokana na majeraha.Carlos Tevez was booed by his own supporters in his first match back from injury on SaturdayAlirejea China hivi majuzi baada ya ziara ya wiki mbili nchini Argentina ambako alikuwa ameenda kutibiwa tatizo la misuli.

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...