Nyota wa mchezo huo alikuwa ni Ibrahim
Ajib ambaye aliandikia Yanga bao la mapema kupitia mkwaju wa adhabu
ndogo dakika ya 24 ambao ulienda moja kwa moja golini. Baadae dakika ya
30 Ajib aliongeza bao la pili na kufanya timu hizo ziende mapumziko
Yanga ikiongoza kwa mabao 2-0.
Kipindi cha pili Yanga walirejea na kasi
ileile wakiendelea kushambulia lango la Stand United ambapo dakika ya
53 kiungo mpya wa timu hiyo Pius Buswita aliipatia bao la tatu timu yake
kabla ya Obrey Chirwa kukamilisha majibu ya Yanga kwa Simba kwa kufunga
bao la 4 dakika ya 69.
Baada ya mchezo nahodha wa mabingwa
watetezi wa timu hiyo Nadir Haroub amesema matokeo hayo yamewaweka
tayari kwaajili ya mchezo wa watani wa jadi jumapili ijayo kwenye uwanja
wa Uhuru jijini Dar es salaam.
Yanga sasa inashika nafasi ya pili nyuma ya Simba zote zikiwa na alama
15 zikitofautiana mabao ya kufunga huku Mtibwa Sugar nayo ikiwa kwenye
nafasi ya 3 ikiwa na alama 15 sawa na Simba na Yanga ikizidiwa mabao ya
kufunga. Mchezo wa wikiendi ijayo ndio utaamua nani aongoze msimamo wa
ligi.
No comments:
Post a Comment