Saturday, 25 November 2017

mayai ya uzazi yatunzwa kwenywe friji

Rita Ora
Rita Ora amefichua kuwa aliweka mayai yake ya uzazi kwenye barafu baada ya miaka 20 alipokuwa akizungumza kwenye kipindi cha Televisheni ya Australia .
Muimbaji huyo wa raia wa Uingereza, ambaye sasa ana umri wa miaka 26 alisemakuwa madaktari walimpenekezea upasuaji wa kuyaondoa mayai hayo mwilini mwake kwasababu " amekuwa akitaka kuwa na familia kubwa".
"Daktari alisema: 'una afya nzuri sasa na itakuwa vema, kwa nini usiyaondoe mayai yako ya uzazi uyatunze , halafu hautakuwa na hofu ya kuwakosa watoto tena ?'," alisema Rita.
Daktari Helen O'Neill, wa chuo kikuu cha London ,anasema: : " Ni bora kuondoa mwilini mwako na kuyatunza mayai yako ya uzazi mapema kuliko kusubiri."
Lakini ni ''hakikisho kamili'' la kupata ujauzuito na wasichana wengi hawawezi kugaramia garama ya upasuaji na utanzaji wa mayai ya uzazi ambayo ni Euro -£5,000 kila mzunguko mmoja wa hedhi.
Rita OraDaktari O'Neil anasema : "Faida za kuyatunza mayai ya uzazi kwenye barafu ni kwamba unachukua jukumu la kutumga mimba mikononi mwako . Kama ukifanyiwa uchunguzi na ikibainika kwamba una uwezo mdogo wa kutpata ujauzito ni vema kuchukua hatua mapema."
Anasema kuna upungufu mkubwa wa mayai bora ya uzazibaada ya mwanamke kufikia miaka 30 - na kwamba ubora huo huendelea kupungua kadri miaka inavyokwenda.
"Bahati mbaya watu wengi huanza kutunza mayai yao ya uzazi wakiwa na umri wa miaka 35, ambapo wanakuwa wamechelewa kidogo ," alielezea.

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...