Saturday, 25 November 2017

robinho afungwa jela

Mshambuliaji wa kimataifa wa Brazil aliyewahi kuvichezea vilabu mbalimbali barani Ulaya kama Real Madrid, AC Milan, Man City na sasa anaichezea Atletico Mineiro ya kwao Brazil Robson De Souza maarufu kama Robinho, leo Alhamisi ya November 23 2017 amehukumiwa kifungo cha miaka 9 jela.
Robinho amehukumiwa kifungo cha miaka 9 jela kwa kuwa miongoni mwa kundi la watu watano waliyohusika na kumdhalilisha msichana raia wa AlbaniaJanuary 22 2013 nchini Italia katika jiji la Milan, wakati huo Robinho na washikaji zake walikuwa Night Club.
Wakati Robinho anatenda kosa hilo alikuwa akiichezea club ya AC Milan ya Italia lakini anayo nafasi ya kukata rufaa na kwa mujibu wa sheria za Italia Robinho kama atakata rufaa hatofungwa hadi rufaa yake isikilizwe kitu ambacho kinaweza kikachukua miaka mingi rufaa hiyo kusikilizwa

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...