Friday, 24 November 2017

viwango vya fifa senegal yapaa

Timu ya taifa ya Senegal, Simba wa TerangaSenegal imepanda hadi nafasi ya 23 kutoka 32 katika orodha ya shirikisho la soka duniani Fifa mwezi Novemba.
Pia wamepanda juu ya Tunisia na Misri na kuwa taifa linaloorodheshwa katika nafasi ya kwanza Afrika.
Hatua hiyo inajiri baada ya Simba hao wa Teranga kushinda mechi mbili dhidi ya Afrika Kusini mnamo mwezi Novemba hatua iliowafanya kufuzu katika kombe la dunia mwaka ujao nchini Urusi.
Nigeria ndio inayoorodheshwa ya chini miongoni mwa mataifa yaliofuzu katika kombe la dunia katika mataifa hamsini duniani na manane kutoka Afrika.
Burkina Faso ndio waliopiga hatua kubwa barani Afrika baada ya kupanda nafasi 11 juu na kufikia nafasi ya 44 duniani na sita katika bara Afrika.
Mataifa yanayoongoza katika orodha hiyo ya Fifa duniani ni Ujerumani, Brazil, Ureno, Argentina na Ubelgiji.
  • 1.Senegal (23)
  • 2.Tunisia (27)
  • 3.Egypt (31)
  • 4.DR Congo (36)
  • 5.Morocco (40)
  • 6.Burkina Faso (44)
  • 7.Cameroon (45)
  • 8.Nigeria (50)
  • 9.Ghana (51)
  • 10.Ivory Coast (61)

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...