Sunday, 3 December 2017

BRIGHTON 1-5 LIVERPOOL: ROBERTO FIRMINO ATUPIA MARA MBILI

Roberto Firmino alifunga mara mbili Liverpool wakirindima kwa ushindi mnono wa 5-1 dhidi ya Brighton katika uwanja wa Amex Stadium.
Mbrazili huyo alifunga goli la kwanza sekunde 79 baada ya Emre Can kufunga goli la kichwa na kuiweka Liverpool mbele kipindi cha kwanza,
Emre Can - Brighton and Hove Albion 1 Liverpool 5: Philippe Coutinho leads Brazilian masterclass as Reds run riot kabla ya kuongeza goli la pili muda mfupi baada ya mapumziko baada ya Simon Mignolet kudaka shuti la Glenn Murray.
Mshambuliaji huyo wa Brighton alifunga kwa mkwaju wa penalti baada ya Jordan Henderson kumsukuma Shane Duffy dakika chache baadaye, lakini Liverpool waliimarisha matokeo yao kwa kufunga magoli mawili dakika za mwishoni.Philippe Coutinho and Jordan Henderson - Brighton and Hove Albion 1 Liverpool 5: Philippe Coutinho leads Brazilian masterclass as Reds run riot
Philippe Coutinho alifunga bao la nne akipiga mpira wa adhabu ndogo chini ya ukuta wa mabeki wa Brighton na mpira ulikwenda moja kwa moja na kuzama wavuni mlinda mlango asijue cha kufanya, na dakika mbili baadaye shuti lake liliguswa na Lewis Dunk aliyejifunga na kuhitimisha karamu ya magoli kwa Liverpool Jumamosi
E. Can (30) Roberto Firmino (31) Roberto Firmino (48) Philippe Coutinho (87) L. Dunk (89 og)

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...