Mchezaji gwiji wa zamani wa Manchester United, Ryan Giggs ameliamsha dude baada ya kusema klabu hiyo ilimpuuza alipotoa ushauri wa kuwasajili wachezaji Gabriel Jesus na Kylian Mbappe.
Giggs amesema wakati huo Mbappe ambaye sasa ni mchezaji ghali wa pili duniani baada ya Neymar, alikuwa anapatikana kwa pauni million 5 kama ilivyo kwa Jesus.
Wakati huo Giggs alikuwa kocha msaidizi chino Louis van Gaal na amesema juhudi zake za ushawishi, hazikuzaa matunda.
Jesus alikuwa akikipiga katika klabu yake ya Palmeiras ya Brazil na alikuwa tayari kujiunga na Manchester United. Kwa sasa Mbrazil huyo ni kati ya nyota tegemeo wa ufungaji katika kikosi cha Manchester City inayotikisa Ligi Kuu England.
No comments:
Post a Comment