Ilikuwa usiku mbaya kwa vijana wa Arsene Wenger baada ya Arsenal kwa mara ya kwanza kumaliza kipindi cha kwanza bila kupiga shuti langoni mwa wapinzani tangu mwezi January.
Bao la Phellipe Coutinho dakika ya 26 la mchezo liliifanya Liverpool kuwa klabu ya 4 kufunga mabao 700+ baada ya Manchester United(840), Arsenal(744) na Chelsea(709),
Baada ya kipindi cha kuanza kuisha ilionekana kama Arsenal wanakufa katika mchezo huo lakini filamu ilianza katika kipindi cha pili ambapo mabao 5 yalifungwa.
Mo Salah aliwapa matumaini mashabiki wa Liverpool akifunga bao la pili na likiwa la 15 kwake msimu huu lakini Alexis Sanchez dakika ya 53 alifufua matumaini ya Arsenal.
Dakika 3 baadae kiungo wa Arsenal Granit Xhaka aliipatia Gunners bao la kusawazisha kabla ya Mesut dakila ya 58 kuiandikia Arsenal bao la 3, dakika ya 71 Roberto Firminho aliufanya mchezo kuwa tatu tatu.
Kwa mabao yaliyofungwa leo yanaifanya Liverpool kuwa timu inayoongoza kwa mabao ya ugenini katika ligi kuu kubwa 5 barani Ulaya wakiwa wamefunga mabao 27 katika mechi 10.
No comments:
Post a Comment