
Katika mchezo huo uliochezeshwa na mwamuzi Alex Muhabi aliyesaidiwa na Okelo Dick wote wa Uganda na Kakunze Herve wa Burundi, Libya ndio waliotawala zaidi na kutengeneza nafasi nyingi, lakini bahati mbaya umaliziaji ukawaangusha.
Tanzania Bara, au Kilimanjaro Stars ya kocha Ammy Ninje haikucheza kwa muunganiko wa kitimu zaidi kila mchezaji alicheza kivyake.
Mbaya zaidi sehemu ya kiungo ilizidiwa na haikuwa na ubunifu kabisa, hivyo kuwapa nafasi Libya kutawala.
Angalau baada ya kuingia Jonas Mkude, sehemu ya kiungo ya Kilimanjaro Stars ilianza kucheza vizuri na hapo ndipo walipoanza kufika kwenye eneo la wapinzani na kupeleka mashambulizi kadhaa.
Katika mchezo wa kwanza wa Kundi A na mashindano kwa ujumla, wenyeji Kenya waliichapa Rwanda 2-0 Uwanja wa Bukhungu, Kakamega, mabao ya Masoud Juma kwa penalti na Otieno Duncan. Amavubi ilimaliza pungufu mechi hiyo baada ya Kayumba Soter kutolewa kwa kadi nyekundu.
Michuano hiyo itaendelea kesho kwa mechi moja ya Kundi B, Uganda wakimenyana na Burundi Kakamega kuanzia Saa 9:00 Alasiri
No comments:
Post a Comment