Sunday, 3 December 2017

Mo dewji aroa ahadi kede kede kwa klabu ya simu soma

Aliyekuwa mfadhili wa siku nyingi wa klabu ya Simba, Mohammed  Dewji 'MO', ameshinda zabuni ya uwekezaji kwenye klabu hiyo katika mchakato uliofanyika leo kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya wekezaji, Jaji Thomas Mihayo ameiambia Goal , kuwa MO ameibuka mshindi baada ya kuwashinda wawekezaji wengine waliojitokeza kuwania nafasi hiyo ya kuimiliki klabu hiyo.
"Katika mchakato wetu Mo pekee aliweka dau la shilingi bilioni 20 kuomba asilimia 50 ya hisa, baada ya klabu kutangaza kuuza asilimia 50 ya hisa zake kwa shilingi za Kitanzania bilioni 20 miezi miwili iliyopita, ingawa baadaye Serikali ikaagiza klabu hiyo isiuze zaidi ya asilimia 49 kwa mtu mmoja," amesema Mihayo.
Kufuatia ushindi huo MO sasa anakuwa muwekezaji wa kwanza kwenye klabu hiyo kongwe nchini na anatarajiwa kuibadilisha klabu hiyo na kuwa ya kimataifa kwa kusajili na kujenga misingi imara ambayo itaifanya klabu hiyo kuwa kubwa kama ilivyo klabu za TP Mazembe na nyinginezo Afrika.
Katika mkutano huo wanachama 1320 walihudhuria mkutano huo kutoka Dar es Salaam na mikoa jirani na kwa furaha ya ushindi huo, Mo Dewji ametoa ahadi 10 za kuleta mabadiliko makubwa.Mohamed Dewji - SimbaMo ameahidi katika mwaka wa kwanza wa uwekezaji wake, ataanza na ujenzi wa Uwanja wa mazoezi wa nyasi za asili na nyasi bandia pamoja na hosteli ya kisasa ya wachezaji.
Amesema, hosteli hiyo itajengwa upya na itakuwa ya kisasa yenye vyumba 35, huku 30 kati ya hivyo vitakuwa kwa ajili ya wachezaji na vitano kwa ajili ya benchi la ufundi na kila kitu ndani.
“Nimefurahi na ninashukuru Mungu kwani kutokana na matakwa yake ndiyo nimefanikisha jambo hili, lakini pia Kamati iliyosimamia mchakato huu kwa ujumla, wanachama na wapenzi wa klabu ya Simba kwa kukubali mabadiliko ya uendeshaji wa klabu,” amesema Mo.
Aidha, Mo amesema Simba itakuwa na gym yake ya kisasa, bwawa kubwa la kuogelea kwa ajili ya mazoezi na sehemu ya kupumzika kwa wachezaji kukiwa Pool table na Play Station , mgahawa kwa ajili ya chakula cha wachezaji, kuanzisha kituo cha kukuzia vipaji kwa vijana akianza na wale wenye umri wa chini ya miaka 14, 16 na 18 na lengo ni kuwakuza.
“Simba itaanza kufanya mambo kimataifa na kushindana na timu kubwa za Afrika kama TP Mazembe na Esperance pia kuitangaza na kuikuza bidhaa yake ikiwa ni pamoja na kutengeneza vifaa mbalimbali kama fulana, kofia, vishika ufunguo na kadhalika,” amesema.

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...