Sunday, 3 December 2017

tetesi za soka ulaya nzima

Mchezaji wa Manchester United Paul PogbaPaul Pogba, ambaye aliwagharimu Manchester United dau lililoweka rekodi ya £89m msimu uliopita wa 2016, anaamini kwamba kiungo wa kati wa Tottenham Dele Alli ana thamani ya zaidi ya £100m. (London Evening Standard)
Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho anataka kumsajili kiungo wakati wa Arsenal na Ujerumani mwenye umri wa miaka 29 Mesut Ozil. (Telegraph)
Liverpool wako tayari kumuuza kiungo wa kati wa Brazil, 25, Philippe Coutinho kwa Barcelona mwezi Januari, lakini iwapo klabu hiyo itatoa dau la £127m. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Mshambuiaji wa Inter Milan raia wa Argentina Mauro Icardi, 24, ana thamani ya Yuro 200m kulingana na ajenti wa mchezaji huyo. (Corriere dello Sport, via BeInSport)
Watford inamlenga mshambuliaji wa Leicester na Algeria mwenye umri wa miaka 29 Islam Slimani. (Watford Observer)
Real Madrid wamezuia usajili wa dau la £38m wa Vinicius Junior na wameamua kumuacha katika klabu yake ya Brazil ,Flamengo kwa msimu mwengine huku kinda huyo mwenye umri wa miaka 17 akitarajiwa kujiunga na klabu hiyo kwa mechi za maandalizi ya msimu ujao mwaka ujao (AS)
Tottenham imekataa kuongeza mishahara ya wachezaji wake licha ya hofu kwamba mazungumzo ya kuongeza kandarasi yamekwama kati ya timu hiyo na beki wa ubelgiji Toby Alderweireld. (Daily Mail)Phillipe Countinho
Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp amechekeshwa na madai kwamba Barcelona imeweka bei ya kumnunua mshambuliaji wa Brazil Philippe Coutinho, 25, katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari. (ESPN)

Mkufunzi wa klabu ya Bournemouth Eddie Howe atafanya mazungumzo na mshambuliaji wa klabu hiyo Lewis Grabban, 29, ambaye yuko katika klabu ya Sunderland kwa mkopo (Bournemouth Echo)

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...