Sunday, 3 December 2017

raisi wa TFF ateuliwa kuwa mjumbe kwenye CECAFA

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia ameshinda nafasi ya Ujumbe wa Kamati ya Utendaji katika Baraza la Soka la Afrika Mashariki na Kati 
(CECAFA).Katika uchaguzi huo uliofanyika leo Desemba 2, 2017 jijini Nairobi, Kenya Rais Karia alipita bila kupingwa baada ya  wanachama watatu kati ya nane kujitoa hivyo watano waliobaki kuchaguliwa bila kupingwa.
    
Wajumbe hao ambao wataungana na Rais wa CECAFA, Mhandisi Mutasim Gafar wa Sudan watakuwa na kibarua cha kuboresha utendaji kazi wa baraza hilo kwa ajili ya kuimarisha soka la Afrika Mashariki na kati.
Wengine waliochaguliwa ni Abdiqaani Arab Said (Somalia), Aimable Habimana (Burundi), Juneid Basha Tilmo (Ethiopia) na Mwanamke Petra Dorris wa Kenya.
source: eatv 

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...