Barcelona wamebainisha kuwa Samuel Umtiti atakosekana kwa muda wa miezi miliwi ijayo baada ya kupata majeraha katika sare ya Jumamosi ya 2-2 dhidi ya Celta Vigo katika uwanja wa Camp Nou.
Umtiti alilazimika kutoka dakika ya 72 kwenye mechi hiyo ya La Liga, na nafasi yaki ilichukuliwa na Thomas Vermaelen.
Barcelona walisawazisha na kuongoza kwenye ardhi ya nyumbani kwao, lakini Celta walipambana na kujipatia pointi moja muhimu nyumbani kwa vinara hao wa ligi.
Miamba ya Catalan wamebainisha baada ya mechi kuwa Umtiti alipata majeraha ya misuli ya paja na mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 hatacheza tena 2017, ikiwa ni pamoja na mechi ya El Clasico dhidi ya Real Madrid Disemba 23.
Umtiti, ambaye alitua Camp Nou akitokea Lyon mwaka 2016, amecheza mechi 17 Barcelona katika kampeni za 2017-18.
No comments:
Post a Comment