
Njia
zinazoweza kukusaidia kuishi bila mkazo (stress): Kutumia likizo ukifanya na
kufurahia mambo mengine tofauti na kazi zako za kila siku. Watu wanaotumia likizo
namna hiyo wana uwezekano mdogo wa kupata maradhi ya moyo kuliko wasiofanya
hivyo

Njia
zinazoweza kukusaidia kuishi bila mkazo (stress): Kusoma habari njema, hadithi
au chochote kinachotia moyo kwa angalau dakika 6, husaidia kupunguza mkazo kwa
68% kulingana na utafiti wa Chuko Kikuu cha Sussex.
. Njia zinazoweza kukusaidia kuishi bila mkazo (stress):
Kusinzia/kulala masaa yasiyopungua nane. Shirikia la Saikolojia la Marekani
@APA linadai mtu asiposinzia vya kutosha anakuwa mwepesi wa hasira hivyo kuongeza
mkazo (stress) 


Njia zinazoweza kukusaidia kuishi bila mkazo (stress): Kuwa
nje ya nyumba na kutembelea mazingira mazuri ni njia ya haraka ya kupunguza
mkazo (stress) na kumfanya mtu kuhisi vizuri. Watafiti wanadai njia hii inaweza
kuwasaidia wagonjwa wa moyo na saratani kuishi umri mrefu zaidi.
No comments:
Post a Comment