Thursday, 25 January 2018

siri kubwa ya biashara yoyote duniani.

Image result for businessHuenda zimeshaelezwa ila sio kwa maneno mepesi sana.

Hizi hapa ukizifuata hakika unatusua vema sana popote duania!

1. Uwepo wa soko

~ Kwamba biashara hio unayotaka kufanya vipi ina soko? Jijibu mwenyewe kwa uhakika.

2. Namna hio biashara utakavyofanya.

~ Chukulia biashara ya elimu. JIULIZE: Je, utawadunga watoto sindano za akili, Je, walimu watakuwa wanafanya exams kwa niaba ya watoto? Je, ada italipwa mara baada ya mtoto kufaulu? kwamba kama hajafaulu, ada asilipe? nk. Lengo, kuja tofauti.

3. Eneo dogo la kufanya biashara.

~ Namaanisha, eneo dogo la kuhudumia. Mfano: Tanzania ina changamoto kubwa sana ya chakula na makazi. Within TZ, DSM ni sehemu yenye changamoto kubwa zaidi. Hadi leo DSM hakuna namna nzuri ambayo wakazi wa DSM wameweza kumudu gharama za chakula na makazi (kodi). Ugumu wa maisha ya DSM ni chakula kuwa juu na kodi. Sasa wewe katika kutanua mabawa Tanzania nzima, unaanza kudili na DSM.

Una faida kubwa ya kupaa kama ndege za Boeing zijui nini kama nini.

Ni hayo tu waungwana ! Mwenye kudaka na adake !

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...