Saturday, 24 March 2018

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah



Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri,, huku mechi hiyo ikiisha kwa Ureno kuondoka na ushindi wa 2-1

Mohamed Salah alianza kwa kufunga goli la kwanza kwa mchezo huo ndani ya dakika 56, na kuifanya Misri iongoze kwa muda wote wa mchezo.

Katika sekunde 120 za mwisho wa mchezo Ronaldo alifunga magoli mawili ya kichwa na kuipa timu yake ushindi.

Mechi nyingne kali ni pamoja na mabingwa wa dunia Ujerumani walipolazimishwa  sare na Hispania na kuifanya mechi hiyo iishe kwa sare ya 1-1

Rodrigo na Muller ndo wafungaji wa magoli katika mechi hiyo.

Jesse Lingard amefunga goli lake la kwanza kwa timu yake ya taifa na ni goli la pekee katika mechi hiyo huku Uingereza wakiondoka na ushindi dhidi ya Uholanzi.


Matokeo ya mechi nyingine ni 
Argentina 2   -  0  Italia 
Ufaransa  2   -   3 Colombia 
Urusi        0    -   3 Brazili 
Japani      1   -    1 Mali

Wednesday, 21 March 2018

Mohamed Salah avunja rekodi ya wakongwe

 Mohamed salehe anaweza kefan ya vitus ambavyo Owen ,suarez na Torres banda ya kuone kuwa vizuri zaidi katika kikosi chake cha Liverpool.
 Salah akiwa na klopp kocha wake baada ya kufunga goli la ushindi.
Mafanikio aliyonayo yeye kwenye Assist na magoli yanaelekea kuwazidi wakongwe waliokuwa na rekodi pale Anfield.

Mo Salah amefikisha magoli 9 kwenye mechi 12 katika michuano ya kufuzu kombe la dunia kitu ambacho mkongwe Robbie Fowler alikuwa na magoli 8 kwa  Idadi ya mechi 12 kwenye michuano kama hii

Tuesday, 30 January 2018

Mtu wa karibu wa Darasa afunguka kuhusu Darasa kuwa Teja

Image result for darasa

Baada ya kimya cha muda mrefu kwa msanii Darassa ambaye mwaka juzi 2016 alitingisha sana na wimbo wake 'Muziki' kumeibuka tetesi kuwa msanii huyo naye amejiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya, jambo ambalo limewashtua wengi.
Kufuatia tetesi hizo mtangazaji wa kipindi cha Bongo fleva Top 20 ya East Africa Radio, Jr Junior alimvutia waya msanii huyo lakini bahati mbaya hakuweza kupokea simu yake jambo ambalo lilimfanya kumpigia simu mtu wake wa karibu ambaye ni producer wake Mr T Touchez ili kufahamu ukweli juu ya tuhuma au tetesi hizo.

Baada ya Mr T Touchez kupigiwa simu alisema yeye hafahamu lolote juu ya jambo hilo na kukiri kuwa kwa sasa hajakutana na msanii huyo muda kidogo, hivyo hafahamu lolote kuhusu hicho kinachoelezwa kutumia dawa za kulevya. 

Nandy asema hatakubali kuunganishwa na mapedeshee wenye pesa bali atawasubiri

Msanii wa muziki wa bongo fleva Nandy ambae anafanya vizuri kwa sasa na wimbo wake wa 'kivuruge' amefunguka na kudai hakuna mtu yeyote atakaeweza kumuunganishia kwa wanaume wenye pesa (pedeshee) bali kama watamuitaji wataenda wenyewe kwake.

Nandy ameeleza hayo kupitia kipindi cha eNewz kutoka EATV baada ya kuwepo tetesi za muda mrefu zinazodai kwamba msanii huyo amesababisha kuvunjika kwa kundi la 'LFLG' kutokana na aliyekuwa meneja wake ambae ni Petit Man kumkuwadia kwa 'vigogo' huku akifahamu tosha kwamba mrembo huyo anatoka kimapenzi na Bill Nas ambae pia alikuwa mmoja wa wasanii katika kundi hilo.

"Mimi mtu hawezi kunipeleka kwa mapedeshe kama kunifuata watanifuata wao wenyewe, hawezi mtu kunipeleka kwa mwanaume sijafikia hatua hiyo. Na sina mazoea na Petit ya kuunganishiana mizigo", alisema Nandy.

Kwa upande mwingine, Nandy amesema haoni umuhimu wa kuongelea mambo ambayo hayana msingi katika kipindi huku akisisitiza kwamba jambo la muhimu kwa sasa ni 'kivuruge' kushika namba moja Tanzania nzima pamoja na wimbo wao mpya na Aslay 'Subalkher'. 

COUTINHO AREJEA LIVERPOOL KUWAAGA WANA

Philipe Coutinho amerejea Liverpool na kuwaaga rasmi rafiki na wafanyakazi wa klabu hiyo.

Coutinho raia wa Brazil amejiunga na Barcelona kwa dau la pauni milioni 145 akitokea Liverpool.

Lakini hakuwa amepata nafasi ya kuwaaga na amerejea ikiwa ni baada ya kucheza mechi moja tu Barcelona ikishinda 2-1.


Mtu aliyekaa naye muda mwingi zaidi alikuwa ni Adam Lallana ambaye amekuwa rafiki yake wakati akiwa Liverpool.

Monday, 29 January 2018

alichokisema sure boy kuhusu kuipenda yanga

Image result for sure boy

Kiungo mshambuliaji wa Azam, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, amesema anawashangaa mashabiki wa timu hiyo wanaodai kuwa yeye ndiyo chanzo cha kufungwa katika mchezo dhidi ya Yanga kwa kuwa ana mpenzi na Yanga, kitu ambacho hakina ukweli wowote zaidi ya kuwa ni uzushi uliokosa tija.
 
Sure Boy kwa sasa ndiyo mchezaji pekee  ambaye amesalia katika timu hiyo tangu ipande Ligi Kuu Bara mwaka 2008 ambapo katika mchezo wa juzi Jumamosi alipata kadi nyekundu dakika ya 81 wakati timu yake ikiwa nyuma kwa mabao 1-2 dhidi ya Yanga katika  mchezo uliopigwa Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

Sure Boy amesema kuwa hashangazwi na maneno ya mashabiki hao, kwa kuwa ana miaka kumi mpaka sasa akiitumia timu hiyo na amekuwa akiambiwa siku zote lakini walipaswa kuangalia mwamuzi alivyoweza kuwamaliza mapema katika mchezo huo.

“Unajua kadi imetokea kwa sababu ni sehemu ya mchezo na Hassan Kessy alitumia udhaifu wa mwamuzi kuweza kunitoa kwa kadi nyekundu, lakini sijui kwa nini watu wote hawakuona kitendo cha kijinga alichokifanya Kessy kwa Joseph Mahundi wakati yupo pale chini, matokeo yake wananiangushia lawama mimi.


“Angalia tangu mpira unaanza, tayari mwamuzi alishaonekana hakuwa na usawa kwa timu zote, ametoa zaidi ya kadi tano kwetu halafu Yanga yule Papy Tshishimbi amecheza rafu muda wote na ngumi akarusha mbele yake halafu wanasema mimi nimewasaidia Yanga, kwani bao la pili limefungwa nikiwa wapi, nina miaka kumi nacheza Azam hivyo siwezi kuwashangaa, zaidi naangalia nitaisaidiaje timu huko mbele,” alisema Sure Boy.

Friday, 26 January 2018

Khan atangaza kurudi kwenye ndondi baada ya kula kichapo May 2016

Amir Khan
Khan hajawahi kuingia ulingoni toka apigwe na  Canelo Alvarez kwenye uwanja wa Las Vegas tangu May 2016.
tangu hapo hajawahi kucheza na alifanyiwa upasuaji kutokana na matatizo ya mkono wake, na amesema hataki mchezo sasa kwakuwa amerudi kwa mbio kali sana kwa yoyote atakayekuwa mbele yake yeye lazima atampiga.
bondia huyu mwenye umri wa miaka 31-ametangaza kurudi katika ndondi kwa mwaka huu wa 2018 na ataanza mapambano yake kuanzi mwezi wa 4 tarehe 21 katika uwanja wa Echo Arena  Liverpool

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...