Saturday, 19 September 2015

Ccm watashtakiwa kwa kosa la kuiba maneno na nembo ya chadema..

CCM Wamekosea Kutumia Neno
na Logo ya M4C Kumnadi
Magufuli

Tangu jana kumekuwepo na mijadala sehemu
mbalimbali kuhusiana na matumizi ya logo ya
M4C kwa chama cha Mzpinduzi (CCM). Wengine
wakisema ni sawa lakini wengine wakisema si
sawa.
Sikutaka kulizungumzia hili lakini naona kuna
upotoshaji (wa makusudi) unaoendelea, hivyo
nimeona nitumie uzoefu wangu ktk taaluma ya
Mahusiano (Public Relations) na uelewa mdogo
wa Sheria nilionao kutoa ufafanuzi juu ya jambo
hili.
Lakini kabla sijaendelea nimpongeze sana
mwanasheria wa CHADEMA John Mallya kwa
kutoa msimamo wa Chama kuwa wataifikisha
CCM mahakamani kwa kitendo cha kurudufu
nembo yao.
Kwa uelewa wangu kinacholalamikiwa si logo tu,
kinacholalamikiwa ni kitendo cha CCM kutumia
nembo ya utambulisho ya chama kingine
(Corporate Identity) ya CHADEMA, while are two
oponent parties.
Muaasisi wa Taaluma ya Public Relations, Arthur
Page alisema ili kutengeneza utambulisho wako
kwa jamii (Corporate Identity) unahitaji kuwa
alama zitakazokutambulisha.
Alama hizo ni pamoja na Nembo (Logo), Jina
(brand name), Rangi (corporate colour), Mundo
wa maandishi (designing) kama ilivyo Cocacola,
etc.
Vyote hivi ndio vinatengeneza kinachoitwa
utambulisho wa kampuni/shirika/asasi/chama
etc.
Nembo ya M4C ni Corporate Identity ya Chama
cha Demokrasia na maendeleo na imesajiliwa
hivyo. Kwa hiyo CCM au chama kingine kutumia
nembo hiyo bila ridhaa au makubaliano maalumu
na CHADEMA ni kosa kisheria (Criminal Fraud).
KWANINI CCM WAMEKOSEA.
Sheria zinazolinda haki miliki Tanzania (The
copyright and neighbouring Act, ya mwaka 1999
na The Trade and Service marks Act, ya mwaka
1986) pamoja na Sheria za kimataifa zinazolinda
haki miliki zinataka kuwe na utouti wa
utambulisho kati ya asasi moja na nyingine,
bidhaa moja na nyingine, shirika moja na jingine
etc.
Utofauti huo unakuwa kwenye maeneo mengi
lakini kwa uchache ni kama ifuatavyo;
1. Jina/Brand name.
Jina moja haliwezi kutumiwa na asasi mbili tofauti
zinazofanya kazi za kufanana. Kwa mfano
Kampuni ya bia ya TBL ikizindua kinywaji
kiitwacho "Burudani" kampuni ya Serengeti
haipaswi kuanzisha kinywaji chenye jina kama
hilo. Sheria inazuia ili kutowachanganya wateja na
kulinda haki ya mwanzilishi wa hiyo "brand
name".
Kwa hiyo kitendo cha CHADEMA kusajili nembo
ya M4C kama "operation brand name" yake
kinazuia chama kingine cha siasa kutumia jina
hilo. Kwa hiyo CCM kutumia M4C ni kosa
kisheria.
2. Muundo/Designing.
Muundo wa maandishi una hati miliki kisheria.
Kwa mfano muundo wa neno Cocacola ulivyo ni
tofauti na muundo wa neno Pepsi. Cocacola
wanaandika kwa kucharaza. Hiyo ni designing
yao. Pepsi hawaruhusiwi kuiga muundo huo
unless kuwe na makubaliano maalumu na
Cocacola.
Sasa CCM kwa ujinga wa kiwango cha "PhD"
wameiga muundo wa neno M4C. Bora hata
wangeandika kwa muundo mwingine, kwa mfano
M-FOR-C, au m4c au namna nyingine
itakayotofautisha brand name yao na ya
CHADEMA. Lakini wamecopy na kupaste. Hapa
haihitaji degree ya sheria kujua kuwa CCM
wamekosea.
3. Rangi/Corporate colour.
Unaposajili bidhaa yako au kampuni yako ni vizuri
kusajili na rangi yako ya utambulisho.
Kwa mfano hati ya usajili ya Chama cha
mapinduzi inatambua rangi za kijani na njano
kama rangi zao za utambulisho (corporate
colour). Chadema rangi zao ni Blue, nyekundu,
nyeupe na nyeusi.
Ukisajili rangi yako ya utambulisho ni kosa
kisheria kutumia rangi ya mshindani wako hasa
kwenye ulimwengu wa leo wa ushindani wa
kimasoko wa "Oligopoly Marketing"
Simba hawaruhusiwi kuvaa jezi za Njano kwa
sababu sio rangi yao ya utambulisho, vivyo hivyo
Yanga kuvaa nyekundu.
Japo Sheria inatoa ruhusa kubadili rangi ikiwa
unaona kuna haja ya kufanya hivyo. Yani ukiona
"clients" wako au "audience" wako hawaridhiki na
rangi yako unaweza kubadili kwa kufuata taratibu
za kisheria. Na si rangi tu bali hata logo au
muundo (design).
Ndio maana Vodacom ilianza na rangi ya Blue na
nyeupe, lakini wakachange na sasa wanatumia
nyekundu na nyeupe. Sheria inaruhusu
kubadilisha.
Lakini CCM hawakufanya hivyo. Bado hati yao ya
usajili inaonesha rangi zao za utambulisho ni
Kijani na Njano, lakini leo wamekurupuka
kutengeneza logo ya M4C kwa rangi ambazo si
zao. CCM hawana utambulisho wa rangi
nyekundu, blue, nyeupe wala nyeusi. Wamezitoa
wapi?
Haihitaji elimu ya sheria kujua hawa watu
wamekurupuka. Yani baba Njano, mama Kijani
halafu mnazaa mtoto mwekundu au mweupe..
haya ni maajabu ya 8 ya dunia.
Haiwezekani baba awe Punda, mama awe Nyumbu
halafu mnazaa mtoto Twiga?? Hakuna "cross
genetics" ya aina hiyo. CCM u have proved
failure.
Nisiwachoshe sana lakini kwa kifupi CCM
wamekurupuka mno. Ni kukosa umakini kwa
kiwango kikubwa. CCM ina wataalamu wa Sheria,
ina wataalamu wa PR and Marketing, ina
wataalamu wa Communication, kwanini
wanafanya "Technical Mistake" ya kitoto namna
hii? Hizi ndio akili za kushauriwa na kina Lusinde
(standard seven) na kupuuza wataalamu. Poor u.!
Malisa GJ.

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...