Mgombea urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli ameombwa kuwafuta kazi baadhi ya viongozi wa chama hicho ambao wamebainika kuwa wanakihujumu kwa kumsaidia mgombea urais wa Chadema, Edward Lowassa.
Katika hali inayoonesha kuwa kuna mchwa wanaokitafuna kwa kificho chama hicho, mjumbe wa kamati ya kampeni ya CCM mkoani Arusha, Victor Njau alimuomba Dk. John Magufuli kuwafukuza kazi mara moja watendaji ambao wanakihujumu chama hicho katika harakati hizi za kampeni.
“Kuna viongozi wanatumia magari ya CCM, wanalipwa mishahara lakini wanaendesha kampeni za kuwaangusha wagombea wa chama tawala. Tunamtaka Dk. Magufuli akishinda aanze na wasaliti hawa,” alisema.
Hii inaonesha kuwa viongozi wanaodaiwa kukisaliti chama hicho wanafahamika na tayari ‘faili’ lao limewekwa sawa wakisubiri adhabu yao mara tu baada ya Dk. Magufuli kuingia ikulu, endapo atachaguliwa na wananchi Oktoba 25, mwaka huu.
Hili sio suala geni kwa mgombea huyo wa urais kwani alishawahi kuweka wazi kuwa anawafahamu baadhi ya watu wanawasaliti kwa kumsaidia mgombea wa Chadema, Edward Lowassa. Aliwakanya watu hao na kuahidi kuwawajibisha pindi atakapoingia madarakani, la sivyo waache usaliti huo. Source: mpekuzi
No comments:
Post a Comment