Wednesday, 25 November 2015

kilimanjaro stars yaifunga Rwanda goli 2 kwa 1 na kuingia robo fainali

Rwanda 1-2 Tanzania: anasema Hamisi, Simon Msuva ameipeleka Kilimanjaro Stars kwenda robo fainali

Tanzania's Kilimanjaro Stars fans cheer their team during a past match. Tanzania on November 24, 2015 sailed through to the Cecafa Senior Challenge Cup quarter-finals after beating Rwanda 2-1 in their Group A match at the Hawassa Stadium. PHOTO | FILE |
mashabiki wa  Kilimanjaro Stars wakiishangilia timu yao katika mechi yao. timu ya kilimanjaro stars ya tanzania imefanikiwa kuingia robo fainali baada ya kuilaza timu ya taifa ya rwanda kwa goli 2 kwa 1 katika uwanja wa  Hawassa Stadium

mchezaji hatari wa Rwanda Jacques Tuyisenge aliwapatia rwanda goli kwenye dakika ya  86, lakini walikuwa wamechelewa.
Katika mechi hiyo iliyopigwa mjini Wassa, Stars ilipata bao moja katika kila kipindi.
Bao la kwanza lilifungwa na Said Ndemla na la pili likatupiwa na Simon Msuva katika kipindi cha pili baada ya kipa wa Rwanda kufanya uzembe.
Stars imefikisha ponti sita baada ya kuifunga Somalia kwa mabao 4-0 katika mechi ya kwanza.
Tayari ina nafasi ya kufuzu, kwani hata timu nyingine katika kundi lake itafikisha pointi 6, bado itakuwa na nafasi, zikifikisha timu mbili, bado itakuwa na nafasi ya best looser.

Mechi ya mwisho ya Kili Stars hatua ya makundi itakuwa dhidi ya wenyeji Ethiopia walioanza michuano kwa kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Rwanda.
Katika mechi ya awali, Zanzibar Heroes iliandikwa mabao 4-0 Uganda ambao walianza michuano hiyo kwa kupoteza kwa mabao 2-0 dhidi ya Kenya.


No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...