Monday, 23 November 2015

ubelgiji yatangaza hali ya wasiwasi

Waziri mkuu wa Ubelgiji Charles Michel amesema kuwa nchi yake  imeweka hali ya tahadhari kwenye mji mkuu Jumatatu huku shule zikifungwa kutokana na tishio la shambulizi la kigaidi, baada ya kufanya kikao na baraza la kitaifa la usalama.
Sehemu zingine za nchi pia zimewekwa katika hali ya tahadhari ya kiwango cha tatu. Afisa wa ngazi ya juu amesema vikosi vya usalama nchini humo vimekuwa vikisaka washukiwa wanaohusishwa na shambulizi la karibuni mjini Paris huku wakazi wa Brussels wakishuhudia ongezeko la askari wanaofanya doria kwenye mitaa .
Njia za reli mjini humo zote zimefungwa leo. Waziri wa mambo ya ndani Jan Jambon amesema mamlaka zina msaka mshukiwa wa shambulizi la Paris Salah Abdeslam anaeaminika kuingia Ubelgiji baada ya shambulizi hilo lililouwa watu 130 pamoja na mashambulizi mengine ya nivemba 13 yaliodaiwa kutekelezwa na Islamic State
source VOA

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...