Yusufu Jumanne Mkazi wa Kihonda alisema kwamba kiongozi huyo anaonesha kwamba ana uwezo mkubwa katika kuongoza taifa kutokana na namna alivyoweza kufanya ziara ya kushtukiza katika ofisi mbalimbali baada kuapishwa.
Amesema kwa hatua hiyo ameweza kufufua matumaini kwa wananchi na kuweza kufanya watumishi wa umma kuwa wachapakazi kutokana na kauli mbiu ya hapa kazi tu.
Naye Emmanueli Victor ambaye ni mwanafunzi katika shule ya msingi Sua amemwomba raisi Magufuli kuweza kuwapa kipaumbele wanafunzi wa shule za msingi kwa kuwalipa walimu madai yao sambamba na kuongeza mishahara ya walimu kwani kufanya hivyo kutawezesha wanafunzi wapate elimu bora
Pia Abou Chongole mkazi wa Magadu alimwomba mheshimiwa Raisi kuweza kutatua matatizo mbalimbali katika mkoa wa morogoro hususani tatizo la mgogoro wa wakulima na wafugaji wilayani kilosa kwani tatizo hili limekuwa sugu kutokana na awamu iliyopita kutotatua tatizo hilo.
No comments:
Post a Comment