Wednesday, 24 August 2016

Japani, China na Korea Kusini zafanya mkutano wa mawaziri

Japani, China na Korea Kusini zafanya mkutano wa mawaziri

Japani, China na Korea Kusini zafanya mkutano wa mawaziri

Mawaziri wa mambo ya nje wa Japani, China na Korea Kusini wamefanya mazungumzo leo Jumatano jijini Tokyo nchini Japani ambapo wamejadiliana masuala ya maeneo.

Waziri wa mambo ya nje wa Japani Fumio Kishida alikuwa mwenyeji wa mazungumzo hayo baina yake na mawaziri wa mambo ya nje Wang Yi wa China na Yun Byung-se wa Korea Kusini.

Mawaziri hao huenda wamejadiliana juu ya suala la nyuklia na majaribio ya urushwaji wa makombora yanayotekelezwa na Korea Kaskazini, pamoja na makubaliano ya biashara huru baina ya nchi hizo tatu.

Viongozi hao pia wamepanga kufanya mkutano wa mmoja mmoja baina yao kujadili masuala ya pande mbili.

Waziri Kishida anapanga kuwasilisha pingamizi kwa waziri Wang Yi wa China kutaka kusitishwa kwa uvamizi wa meli za China wa mara kwa mara kwenye eneo la maji la Japani jirani na visiwa vya Senkaku.

Japani inadhibiti visiwa hivyo na serikali ya nchi hiyo imeendelea kusisitiza kuwa visiwa hivyo ni sehemu ya eneo la urithi la Japani. China na Taiwan zinadai kuvimiliki.
source: NHK

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...