Tuesday, 13 September 2016

je? ni kwamba kisasi kitalipwa au vipi?

psg-vs-arsenalMara ya mwisho Arsenal kucheza dhidi ya PSG kwenye dimba la Parc des Princes ilikuwa ni msimu wa 1993/1994.
Shukrani kwa mshambuliaji wa Arsenal Ian Wright ambaye alifunga bao pekee siku hiyo ambalo lilitosha kuipeleka Arsenal hatua ya fainali ya iliyokuwa michuano ya washindi barani Ulaya.

Arsenal ilikuwa chini ya kocha George Graham ambaye alifanikiwa kushinda ubingwa  pekee wa michuano ya ngazi ya vilabu barani Ulaya  baada kuifunga Parma kwenye mchezo wa hatua ya fainali ya washindi.
Siku ya Jumanne ya wiki hii timu ya Arsenal inaanza kampeni  za michuano ya Uefa.
 Inakutana na PSG kwenye mchezo wa kwanza wa kundi A hatua ya makundi kwenye uwanja wa Parc des Princes ikiwa imepita miaka 22.  Je upi uwezekano kwa PSG kupata ushindi?

HALI YA VIKOSI ARSENAL
 
Ushindi dhidi ya Southampton wikiendi iliyopita utaongeza ari ya kujiamini kelekea mchezo huu. taarifa ya kurudi beki Laurent Koscielny ambaye alipata jeraha la kichwa kutasaidia kuimarisha safu ya ulinzi ya Arsenal akicheza sambamba na Shkodran Mustafi.

Moja ya wachezaji wa kuchungwa na PSG ni kiungo wa Arsenal Santiago Cazorla ambaye amechangia magoli manne hadi sasa kwenye EPL. Amefunga mawili na kutoa pasi mbili za mabao.
Rekodi zinaonekana kuibeba Arsenal inapocheza na timu za Ufaransa baada ya kufanikiwa kushinda mechi saba za siku za karibuni ambazo zilichezwa kwenye ardhi ya Ufaransa

 PSG
Psg itaingia kwenye mchezo huu ikiwa na kumbukumbu ya kutoka sare 1-1 dhidi ya St Entiene kwenye mchezo wa ligi kuu mwishoni mwa wiki iliyopita. Wapo katikati ya msimamo wa ligi baada ya kukusanya point saba kwenye michezo minne.

Wachezaji Angel Di Maria, Lucas Moura na Edson Cavanni wamekuwa na mwanzo mzuri hivyo wanaweza kuwa na madhara zaidi kwa upande wa Arsenal.

Kocha Unia Emery alifanya vizuri akiwa na Sevilla ya nchini Hispania. Baada ya kutwaa mataji matatu ya Europa League, atakuwa kwenye mtihani wa kwanza ngazi ya michuano ya Ulaya bila majina makubwa ya msimu uliopita zlatan Ibrahimovic na David Luiz.

UTABIRI
Unai Emery aliwapumzisha baadhi ya nyota wake kwenye mechi dhidi ya St Entiene ili kukusanya nguvu kwa ajili ya mchezo huu. Arsene Wenger ametumia dirisha la usajili kuimarisha kikosi chake. Pia anabebwa na rekodi dhidi ya timu za Ufaransa kwa siku za karibuni.
PARIS SAINT GERMAIN 1–2 ARSENAL

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...