Thursday, 15 September 2016

madereva wa tanzania watekwa nchini CONGO.



Baada ya Taarifa kusambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu utekwaji wa madereva kutoka Tanzanjia huko Congo, Leo September 15 2016  taarifa imetolewa na serikali kupitia wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Taarifa hiyo imesema kwamba Serikali imepokea juu ya kutekwa kwa malori 12 katika eneo la Namoyo jimbo la Kivu Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mnamo September 14, 2106. Taarifa imesema kuwa kati ya malori hayo, nane yanamilikiwa na mfanyabiashara Azim Dewji na mengine yanamilikiwa na wafanyabiashara Kenya.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo ni kwamba waliofanya utekaji ni kikukndi cha waasi cha MaiMai na baada ya utekaji magari hayo, waliwashusha madereva na kuwapeleka porini kisha kuyateketeza kwa moto malori manne ambayo yote ni ya Dewji.
Watekaji hao walitoa saa 24 kuanzia kuanzia jioni ya September 14 wakitaka walipwe fedha kiasi cha dola za Kimarekani 4,000 kwa kila dereva ili waweze kuwaachia pia walitishia kuwaua mateka hao endapo hawatalipwa kiasi hicho cha fedha walichokitaka mpaka kufikia jioni ya September 15.
Taarifa za awali zimedai kuwa madereva wawili kutoka Tanzania walifanikiwa kutoroka na ndio waliotoa taarifa za kuhusu tukio hilo. Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki imesema imeshachukua hatua za awali za kuwasiliana na Serikali ya DRC ili kuhakikisha kuwa madereva hao wanaachiwa iwezekanavyo wakiwa salama kabisa.

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...