Friday, 3 March 2017

Askofu Gwajima Amvaa Makonda Kuhusu Vyeti vyake

Siku moja baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kusema kuwa hawezi kujibu madai ya mitandao ya kijamii kuwa alitumia vyeti vya mtu cha kidato cha nne, Askofu Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima ameibuka na kusema kuwa ni kweli alitumia vyeti hivyo.
Askofu Gwajima amesema kuwa anamfahamu sana Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na kuwa jina lake halisi ni Daudi Bashite na kwamba hilo la Paul Makonda ni la mwenye vyeti hivyo.
Aidha, Askofu Gwajima amedai kuwa anavyovyeti vya Daudi Bashite vinavyoonyesha kuwa hakufaulu na kwamba atashangaa kama Waziri wa Elimu, Prof. Ndalichako atalifumbia macho jambo hili. 
Pia ametishia kuwa, kama mamlaka husika hazitachukua hatua haraka basi yeye atatoka hadharani na vyeti hivyo.


source: Muungwana

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...