Sunday, 19 March 2017

Arsenal yatwangwa magoli matatu kwa moja

Arsenal ilipata pigo la nne katika mechi tano za ligi baada ya mabao mawili ya Craig Dawson kuisaidia West Bromwhich Albion kuilaza timu hiyo ya Arsene Wenger kwa mabao 3-1.
vikosi vya klabu hizi mbili ni: 
WEST BROM: Foster 7; Dawson 8.5 (MoM), McAuley 7.5, Evans 8, Nyom 7.5; Livermore 7.5, Fletcher 7.5; Chadli 7.5 (Field 90’), Brunt 8 (Yacob 72’), McClean 7.5; Rondon 6 (Robson-Kanu 54’ 6.5)
akiba ambao hawakutumika: Myhill; Olsson, Wilson, Leko.
MANAGER: Tony Pulis 8 
magoli: Dawson 12, 75; Robson-Kanu 55
BOOKINGS: McClean
ARSENAL: Cech 4 (Ospina 38’ 4); Bellerin 5, Mustafi 5, Koscielny 5; Monreal 5; Oxlade-Chamberlain 5, Xhaka 5; Walcott 5.5 (Giroud 65’ 5), Ramsey 5, Sanchez 6 (Iwobi 78’); Welbeck 5. Arsene Wenger 5
 akiba ambao hawakutumika: Mertesacker, Gabriel, Coquelin, Elneny.
MANAGER: Arsene Wenger 5 
goli: Sanchez 15
watazamaji: 24,065 (2,766)
muamuzi: Neil Swarbrick 
Dawson alitumia fursa ya makosa yaliofanywa na walinda lango la Arsenal kufunga mabao yake yote mawili kwa kichwa kupitia kona zilizopigwa na hivyobasi kuathiri uwezo wa Arsenal wa kumaliza katika timu nne bora.
Awali Arsenal ilikuwa imejikakamua baada ya kuwa bao moja chini ,na kusawazisha kupitia Alexi Sanchez likiwa bao la 18 la mchezaji huyo wa Chile msimu huu.
Hatahivyo walisalia nyuma kwa mara ya pili dakika kumi za kipindi cha pili baada ya mchezaji wa ziada Hal Robson Kanu kufunga bao, dakika mbili tu baada ya kuingia.
Arsenal ambayo ilimpoteza kipa Petr Cech kupitia jeraha walikabiliwa na kutawaliwa na kushindwa kupata bao la pili.
Na mwisho wamechi hiyo mashabiki wa timu ya Arsenal waliendelea jitihada za za kumtaka kocha wa klabu hiyo kufutwa kazi kwa matokeo mabaya.
Walibeba mabongo yaliomtaka kocha huyo kuondoka






No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...