Na Zainabu Rajabu
NAHODHA msaidizi wa timu ya Tanzania (Taifa stars) Himid Mao amesema
mechi dhidi ya Botswana ilikuwa nzuri kwa pande zote mbili, huku timu
zote zikishambuliana kwa zamu.
Himid Mao pamoja na Jonas Mkude waliteuliwa kuwa manahodha wasaidizi
wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kutoka na aliyekuwa nahodha
msaidizi John Bocco nje ya timu baada ya kusumbuliwa na majeraha.
Akizungumza na Shaffihdauda.co.tz Himid Mao amesema: Tulicheza vizuri
licha ya kuwa na makosa madogomadogo ambayo mwalimu akikaa
atayarekebisha ili mchezo ujao dhidi ya Burundi yasijirudie.”
“Kwasasa timu ina mabadiliko makubwa sana kutoka na mwalimu Mayanja
kutoa nafasi kubwa kwa chipukizi kama Gabriel Michael, Hassan Kabunda,
ambao nawaona wakipewa nafasi wataweza,” alisema Himid.
Aidha Himid Mao ambae ni Nahodha msaidizi Azam Fc alisema kuwepo kwa
Mbwana Samatta na Farid Mussa katika timu ya Taifa ni kitu kikubwa kwao
na pia ni fundisho kwa wachezaji wengi ambao wana ndoto za kucheza soka
la kulipwa.
No comments:
Post a Comment