Sunday, 26 March 2017

samata aifungia taifa stars magoli mawili ya ushindi katika mechi yakirafiki dhidi ya taifa stars na botswana



Nahodha wa Taifa Stars, Mbwana Samatta amefunga mabao mawili na kuiwezesha Taifa Stars kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Botswana.

Samatta alifunga bao la kwanza katika dakika ya kwanza tu katika mechi hiyo ya kirafiki katika kalenda ya Fifa.


Bao hilo lilidumu hadi kipindi cha kwanza. Kipindi cha pili Botswana nao walionyesha uhai lakini Stars walikuwa imara.

Mara kadhaa, kipa wa Botswana, alionyesha umahiri na kuokoa mikwaju kadhaa.



Samatta alishindilia bao la mwisho zikiwa zimebaki dakika chache akipiga mkwaju matata wa adhabu.

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...