Saturday, 18 March 2017

Manchester city kufanya usajili wabeki Antonio Rudiger kutoka Roma


beki wa ROma yupo katika mipango ya kocha pepe guardiola katika mpango wake wa kuimarisha ukuta wake.

Rudiger atasajiliwa kwa kitita cha £30million katika msimu ujao, manchester city wako katika hatua za mwisho kuhakikisha wanampata beki huyu.

City tayari wameshapeleka waangalizi katika klabu hiyo kwa ajili ya kumfuatilia na wameonyesha kuwa mchezaji huyu yuko vizuri na ataweza kujiunga na klabu  hiyo msimu ujao.
klabu ya Chelsea nayo inaonekana kumfuatilia mchezaji huyu kwa ajili ya kumsajili lakini klabu inayoonekana kuwa na na nafasi nzuri ni man city kwakuwa wameshafanya hatua za mwanzoni kabisa japo chelsea wanaonekana kama kumtafuta mchezaji mwingine.
Roma's defender from Germany Antonio Rudiger (L) vies with Lazio's defender from Netherlands Stefan de VrijGuardiola anamchukua kwa ajili ya kujazia pengo la mabeki na kushirikia na Stones kuimarisha ulinzi klabuni hapo. 
Rudiger ni mchezaji ambaye anaweza kucheza pembeni pia na katikati kitu ambacho kinampa furaha guardiola kwa ajili ya kumtumia kwa kuwa man city ni klabu inayoonekana kukosa ulinzi imara
 
 

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...