Saturday, 18 March 2017

Yaya toure kujiunga na manchester united msimu ujao


YAYA TOURE aanzisha tena zengwe katika klabu yake ya man city baada ya kuonekana kutaka kuihama klabu hiyo.

meneja wake Dimitri Seluk  ameshahusisha uhamisho huo na klabu ya manchester united.
yaya toure ni moja kati ya wachezaji 6 ambao mkataba wao unaisha mwisho wa msimu huu japo yeye hajazungumza na klabu hiyo kuhusu kuongeza mkataba.

Wakala wake amesema kocha Morinho ni mzuri maana anajua kuwatumia wachezaji kama ameweza kumtumia ibrahmovic hawezi kushindwa kumtumia yaya toure na tena walicheza wote wakiwa Barcelona

najua hawa ni wapinzania lakini sio tatizo kwangu au kwa yaya bali tatizo ni kwao hao man city staff.

kocha Guardiola akiongea na yaya toure

yaya akiongea na SKY sport alisema " mimi nilikuja hapa kwa ajili ya kucheza na kuionyesha dunia kile nilichonacho na pia kukaa na wenzangu vizuri tupige stori, japo mashabiki na wanachama hawakuamini maneno yangu kwamba tutaifanya klabu hii kuwa kubwa"

mchezaji huyu mwenye miaka 33 amekuwa hana amani katika klabu yake hiyo hivyo anaona ni vyema atafute sehemu nzuri ya kucheza japo alihusishwa kuamia nchini china lakini yeye mwenyewe alikataa na kusema bado ananguvu na uwezo wa kucheza katika klabu za uingereza.

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...