Sunday, 19 March 2017

Samatta aendeleza mauaji yake huko KRC genk baada ya kufunga goli la kuongoza kwa timu yake

NAHODHA wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta jana amefunga bao la kwanza timu yake KRC Genk ikishinda 4-0 Uwanja wa Het Kuipje dhidi ya wenyeji, KVC Westerlo katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji.
Samatta, mshambuliaji wa zamani wa Simba SC ya Dar es Salaam, alifunga dakika ya saba tu akimalizia pasi ya kiungo Mspaniola, Alejandro Pozuelo Melero.  
Na mabao mengine ya Genk yakafungwa na kiungo Mbelgiji, Thomas Buffalo dakika ya 27, beki Mgambia, Omar Colley dakika ya 61 na kiungo wa Ukraine, Ruslan Malinovskyi dakika ya 90 na ushei.
Mbwana Samatta jana amefunga bao la kwanza timu yake KRC Genk ikishinda 4-0 Ubelgiji 

Samatta akipongezwa baada ya kufunga jana

Samatta jana amefikisha mabao 17 katika mechi 48 alizoichezea Genk tangu asajiliwe Januari mwaka jana kutoka TP Mazembe ya DRC.
Kati ya mechi hizo 48, michezo 18 Samatta alicheza msimu uliopita na 30 msimu huu na kati ya hiyo, ni michezo 29 tu ndiyo alianza, 10 msimu uliopita na 19 msimu huu.
Mechi 19 kati ya hizo alitokea benchi, nane msimu uliopita na 11 msimu huu, wakati 11 hakumaliza baada ya kutolewa, sita msimu uliopita na tisa msimu huu na katika mabao hayo 17, 10 amefunga msimu huu na sita msimu uliopita.
Kikosi cha KRC Genk kilikuwa: Ryan, Castagne, Brabec, Colley, Uronen/Walsh dk45, Berge, Malinovskyi, Pozuelo/Naranjo dk72, Boetius, Buffalo/Trossard dk79 na Samatta.
KVC Westerlo: From Langendonck, Apau, Daems, Annys, De Ceulaer/Acolatse dk31, Hyland, Schuermans/Strandberg dk31, Christensen, Heylen, Hamada na Ganvoula.

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...