Sunday, 19 March 2017

Mbao ni timu ya kwanza kutinga fainali FA

Salmin Hoza alianza kumtungua mchezaji bora wa Ligi Kuu Januari kwa shuti la mbali dakika ya 42  kabla ya Dickson Ambundo kufunga la pili dakika ya 84.
Mshambuliaji wa zamani wa Mtibwa Sugar, Azam FC na Simba, Ame Ali ‘Zungu’ akaifungia Kagera bao la kufutia machozi dakika ya 92.
Michuano hiyo itaendelea kesho kwa mchezo mmoja kati ya Simba SC na wenyeji Madini FC Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.
Mechi nyingine za Robo Fainali kati ya Azam FC na Ndanda FC Uwanja wa Azam Complex, Chamazi na Yanga dhidi ya Prisons ya Mbeya Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam zitapangiwa tarehe.
Bingwa wa michuano hiyo kwa mujibu wa kanuni, atazawadiwa Sh. Milioni 50 na ndiye atakayeiwakilisha nchi kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika, wakati bingwa wa Ligi Kuu atacheza Ligi ya Mabingwa Afrika

source:zubery

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...