BEKI wa Jamhuri ya Ireland Seamus Coleman amevunjika mguu kwenye mchezo
uliomalizika kwa sare ya bila kufungana dhidi ya Wales kwenye uwanja wa Aviva
usiku wa kuamkia leo.
Beki huyo wa Everton 28, aliwekewa oksijeni kabla ya kutolewa kwa machela
baada ya kugongwa na Neil Taylor ambaye nae alitolewa nje kwa kadi nyekundu.
Tukio hilo lilitokea kipindi cha pili dakika ya 69 katika mchezo huo muhimu
wa kufuzu kwa fainali za kombe la dunia ambapo kocha Martin O’Neill wa Jamhuri
ya Ireland alisema “amevunjika vibaya”.
“Seamus amepelekwa hospitali na daktari amethibitisha amevunjika mguu,”
aliongeza O’Neill.
“Ni hasara kubwa kwa Everton, hasara kwetu pia. Lakini ni matumaini yangu
atapambana na atarejea uwanjani.”
Kwa upande wake Meneja wa
Wales Chris Coleman alisema beki wake Taylor hakufanya jambo zuri.
Wales Chris Coleman alisema beki wake Taylor hakufanya jambo zuri.
“Tulimwambia hakufanya jambo zuri kabisa, ndiyo maana tunaomba radhi.
“Taylor sio mchezaji wa aina hiyo ila alitumia nguvu kubwa kupambana na
Seamus. Sikutazama tukio hilo tena.”
Everton wanarejea kwenye mikikimikiki ya ligi kuu nchini Uingereza na
Jumamosi ya Aprili mosi ambapo watashuka dimbani kucheza na wapinzani wao
wakubwa Liverpool kwenye uwanja wa Anfield.
Sare hiyo imeifanya Jamhuri ya Ireland kushuka kileleni mwa msimamo wa kundi
D baada ya Serbia kuifunga Georgia siku ya Ijumaa ambapo Wales wapo nafasi ya
tatu wakiwa nyuma kwa alama nne dhidi ya vinara.
Mechi inayofuata kwa Jamhuri ya Ireland kwenye kundi hilo itakuwa Juni 11
dhidi ya Austria.
No comments:
Post a Comment