watu walihofu wakijua Hazard angeachwa katika mchezo huu lakini baada ya kuonekana na kung'aa kwenye mchezo huo.
Wachezaji wa chelsea wakishangilia baada ya kufungwa goli la ushindi kwa timu yake
Mchezaji wa Chelsea Nemanja Matic alifunga bao zuri kutoka mbali na kuisaidia timu yake kuinyamazisha Tottenham katika nusu fainali ya Kombe la FA katika uwanja wa Wembley.
Chelsea iliizaba Tottenham mabao 4-2 na hivyobasi kujikatia tiketi katika fainali ya kombe hilo dhidi ya mshindi wa nusu fainali ya pili kati ya Arsenal dhidi ya Manchester City.
Willlian aliiweka mbele Chelsea kunako dakika ya sita kwa kupiga mkwaju wa adhabu kabla ya kuongeza la pili kwa njia ya penalti kabla ya kipindi cha kwanza kukamilika.
Harry Kane alikuwa amesawazisha kutoka kwa krosi iliopigwa na Christian Ericksen kwa Suprs ambao walisawazisha tena kupitia bao la Delle Ali.
Mchezaji wa ziada Eden Hazard aliiweka Chelsea mbele kwa mara ya tatu kabla ya Matic kufunga bao la nne na kuiweka kifua mbele Chelsea.
wanyama ndie mchezaji aliyeonekana kuwa na uhai kwa timu ya totenham kwa kuwazuia wachezaji wa kati kushindwa kuchezea mpira
kabla mpira haujachezwa timu zote zilikuwa katika majonzi ya kuondokewa na mchezaji huyu wa kimataifa wa uingereza na aliichekuwa kocha wa klabu ya watoto wa totenham
No comments:
Post a Comment