Saturday, 22 April 2017

mtanzania anayecheza katika klabu ya PSG ya ufaransa anena kuhusu mchezaji wa serengeti boys

Mtanzania anaecheza katika timu ya vijana ya PSG ya Ufaransa Hytham Saduun ameiambia Mtibwa News kwamba, anamkubali nyota wa Serengeti Boys Nickson Clement Kibabage na kumtabiria kufika mbali.
Kibabage kwa sasa yupo nchini Morocco na kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ wakijifua kujiandaa na michuano ya AFCON kwa vijana wa U-17 inayotarajia kuanza Mei 14, 2017 nchini Gabon.
“Kibabage ana kipaji kikubwa atakuja kuwa mchezaji mkubwa,” anasema Hytham ambaye aliwahi kucheza kwenye kikosi cha U-20 cha Mtibwa Sugar.
Kabla ya kufika PSG, Hytham alitoka Mtibwa Sugar na kwenda Dubai ambapo aliwavutia mawakala walioamua kumpeleka kujiunga na PSG ya Ufaransa.
......

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...