Kati ya makocha wanaohusishwa na kuibeba mikoba ya Arsene Wenger ni Jorge Sampaoli,sio tu Arsenal bali pia uwezo wa Sampaoli umemfanya ahusishwe pia na timu kubwa kama Barcelona na Real Madrid.
Sampaoli ambaye aliiongoza Chile kuchukua kombe la Copa Amerika kwa mara ya kwanza ameeleza nia yake ya kufundisha soka katika ligi ya EPL.
Hii inaweza kuiamsha Arsenal kwani watu wengi wanataka Wenger aondoke Arsenal, lakini hofu kubwa kwa mashabiki wengi wa klabu hiyo ni nani atayemrithi Wenger kama akiondoka katika klabu hiyo.
“Natamani kupeleka ujuzi na uzoefu wangu Uingereza, unajua Uingereza makocha wengi wazuri wameshapeleka ujuzi wao na mifumo yao na wengi ni makocha bora, na mimi nataka kushindana nao” alisema Sampaoli.
Samapaoli jina lake lilikuwa kubwa akiwa na Chile lakini msimu huu pia na Sevilla alivichachafya vigogo vikubw vya Hispania timu ya Barcelona na Madrid na kukaa katikati yao katika msimamo wa ligi.
Mizuka yake anapokuwa kwenye eneo lake uwanjani ni kati ya vitu mashabimi wengi wanatamani kukiona kikija Uingereza ili akaungane na makocha wa aina yake akiwemo Jurgen Klopp na Antonio Conte.
Sampaoli amesema bado anajifunza lugha ya kiingereza ili kama simu akahamia katika nchi hiyo asipate tabu kuzungumza lugha hiyo lakinj pia ameeleza kwamba kabla ya Antonio Conte kutua Chelsea, mmiliki wa klabu hiyo Roman Abromovich alimfuata na kutaka awe kocha wa Chelsea.
Kama ivyo kwa Conte, Sampaoli ni kocha ambaye ana mbinu sana uwanjani na anabadilisha kila dakika, alipokuwa Chile alikuwa maarufu kwa mfumo wake wa 3-3-1-3 ambao ulimpa kombe la Sudamericana, inawezekana Sampaoli ni mrithi wa Wenger? Tusubiri mda utaeleza.
No comments:
Post a Comment