Sunday, 9 April 2017

wachezaji wa real madrid wamkataa ronaldo kwenye kikosi

Taarifa kutoka ndani ya klabu ya Real Madrid zinasema hali sii nzuri kwa mwanasoka bora wa dunia Cristiano Ronaldo kwani baadhi ya wachezaji wenzake hawataki acheze.
Ripoti zinasema kabla ya mchezo kati ya Real Madrid dhidi ya Atletico Madrid, baadhi ya wachezaji wa Real Madrid walimfuata kocha mkuu wa klabu hiyo Zinedine Zidane na kumuomba Ronaldo asicheze katika mchezo huo.
Inadaiwa Gareth Bale ndio aliongoza kundi hilo la wachezaji wa Real Madrid waliomfuata Zidane huku pia wachezaji wengine akiwemo Luka Modric na kiungo wa timu hiyo Toni Kroos nao walikuwa pamoja na Bale kujaribu kumuomba Zidane asimpange Ronaldo.
Inadaiwa wachezaji hao wa Real Madrid wamechoshwa na kiwango cha mchezaji huyo, wengi wanaamini Ronaldo kiwango kimeshuka sana na ndio sababu inayopelekea Real Madrid kupata tabu katika mbio za ubingwa.
Lakini pia kuna wachezaji wazawa wa Hispania akiwemo Alvaro Moratta nao hawavutiwi na mpango wa Zidane kumuanzisha Ronaldo kila siku huku wenyewe wakiwa kwenye benchi tu kila mchezo.
Hata hivyo Zidane alimuanzisha Ronaldo katika mchezo huo ambao uliisha kwa suluhu ya bao moja kwa moja, Ronaldo yuko katika hati hati ya kuukosa mchezo dhidi ya Barcelona kwani ana kadi mbili za njano na endapo ataruhusu kadi nyingine ya njano katika mchezo ujao atakuwa na jumla ya kadi 3 za njano mfululizo, na hiyo itamfanya kuikos El Classico.
Endapo Ronaldo ataukosa mchezo wa El Classico baasi mchezo huo utachezwa bila nyota wakubwa wawili, kwani Barcelona nao watamkosa Neymar ambaye atakuwa anatumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyoipata katika mchezo dhidi ya Malaga.

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...