Wednesday, 12 April 2017

WACHEZAJI WATANI ANAOWATAKA WENGER KATIKA USAJILI UJAO AKIPEWA PAUND MIL.200

klabu ya arsenal inataka kumpa kocha wake pesa ya usajili kwa mwezi wa januari kwa ajili ya kuimarisha kikosi chao, pamoja na kwamba kocha huyo hajafanya vizuri katika michuano ya msimu huu lakini uongozi unataka kumpa paund milioni 200 kwa ajili ya usajili.

kocha huyo anataka kwasajili wachezaji watano vijana kwa ajili ya kuimarisha kikosi.
wachezaji wanaoonekana kuondoka msimu ujao ni  Mesut Ozil, Jack Wilshere, Alex Oxlade-Chamberlain, Olivier Giroud, Lucas Perez na David Ospina. 

Moussa Dembele

Mchezaji huyu ameifungia timu yake ya Celtic magoli 32 msimu huu. mchezaji huyu amekuwa muhimu sana katika klabu yake hiyo kwa msimu huu. 
mchezaji huyu ananyemelewa na klabu nyingi za ulaya.
mchezaji huyu wa miaka 20 bado anamuda wa kucheza mpira zaidi.

Kieran Tierney

kiungo huyu wa miaka 19 anayeichezea klabu ya celtic kwa nafasi ya kiungo wa kushoto nyuma anafanya vizuri katika klabu yake. Na kocha wa arsenal anawapenda wachezaji wenye umri mdogo hivyo nafasi ni kubwa kwa mchezaji huyu.

Jordan Pickford

goli kipa wa klabu ya sunderland anaonekana kuwa na nafasi kubwa katika klabu ya Arsenal baada ya kuonyesha kiwango cha juu. 

Wilfried Zaha

mchezaji huyu itakuwa ni uhamisho wake mkubwa baada ya kuhamia Manchester united na kuonekana kukosa nafasi kwa mwaka 2013 lakini baada ya kuhamia klabuni hapo anaonekana kuwa muhimu sana 
mchezaji huyu mwenye umri wa miaka 24 amefunga 6 na kusababisha magoli 11 kwa michezo 28 alizocheza.

Alexandre Lacazette

mfaransa huyu anaonekana kuwa na kiwango kizuri katika klabu yake ya lyon na kufunga magoli 30 kwa michuano yake yote aliyocheza hapo.

No comments:

Featured Post

Ronaldo kaonyesha yeye ni mwamba dhidi ya Salah

Mchezaji  wa klabu ya Real Madrid na nahodha wa timu ya taifa ya Ureno amefunga magoli mawili  (2) katika mechi kati ya Ureno na Misri...