Real Madrid wanafikiria kumuuza mshambuliaji Gareth Bale, 27, ili kupata fedha za kumnunua Kylian Mbappe, 18, kutoka Monaco. (Sunday Express)
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger anaamini Kylian Mbappe atabakia Monaco kwa msimu mmoja zaidi. (Sun on Sunday)
Dau la Chelsea la pauni milioni 88 la kumtaka mshambuliaji wa Juventus Gonzalo Higuain, 29, limekataliwa. (Tuttosport)
Kuna wasiwasi kuhusu hatma ya meneja wa Chelsea Antonio Conte, 47, baada ya mazungumzo ya mkataba mpya kusuasua. (Sun on Sunday)
Liverpool wanatarajiwa kupanda dau jipya kutaka kumsajili kiungo wa RB Leipzig, Naby Keita, 22 wiki ijayo, baada ya dau la pauni milioni 57 kukataliwa. (Sunday Mirror)
Kumekuwa na wasiwasi zaidi kuhusiana na mustakbali wa Alexis Sanchez, 28, baada ya kusema anataka kucheza Klabu Bingwa Ulaya. (ESPN)
Manchester City wanaongeza juhudi zao za kutaka kumsajili beki wa kushoto wa Monaco, Benjamin Mendy, 22, kwa pauni milioni 50 hii ni baada ya Tottenham kukataa kuwauzia Danny Rose, 27. (Sunday Express)
Stoke City wanasubiri West Ham kupanda dau la tatu kutaka kumsajili Marko Arnautovic, 28. Stoke wanataka pauni milioni 22.5. (Mail on Sunday)
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amesema kiungo Alex Oxlade-Chamberlain, 23, atabakia Emirates, licha ya Liverpool kumtaka. (Metro)
Leicester City wanataka pauni milioni 40 kumuuza Riyad Mahrez, 26, kwenda Roma. Chelsea na Everton pia wanamtaka winga huyo. (Mail on Sunday)
Riyad Mahrez tayari amekubaliana na Roma. (Mediaset)
Beki wa kulia wa Real Madrid, Danilo, 26, anataka kuhamia Chelsea. (Diario Gol)
Manchester City nao wamejiunga katika mbio za kutaka kumsajili beki wa kulia wa Real Madrid Danilo, 26, ambaye thamani yake ni takriban pauni milioni 21.9. Chelsea na Juventus wanamtaka pia beki huyo kutoka Brazil. (Sunday Times)
No comments:
Post a Comment